HISTORIA YA USAFIRI WA ANGA NA WALIO GUNDUA NDEGE.

Orville pamaja na ndugu yake Willbur

Mwaka 1700 binadamu alifikilia kuwa anaweza kutengeneza mashine ambayo itaweza kuruka na akaiendesha hii ni kutokana na wivu alipo ona ndege (Birds) wakiruka. Mwaka 1784 binadam alitengeneza Pulizo kubwa (Ballon Hot chair) ambalo ndio ilikuwa chombo cha kwanza cha anga ambacho kinaongozwa na binadamu katika historia ya mambo ya anga Na kwa mara ya kwanza Pulizo hilo liliruka America. Licha ya kufanikiwa kutengeneza Pulizo hilo hawakulizika kutokana ilikuwa ni ngumu kuliongoza lilielekea upepo unapo elekea.
      Tarehe 17/12/1903 North Carolina Malekani Wilbur Wright pamoja na ndugu yake Orvile  Wright waliingia katika historia ya mambo ya anga baada ya kutengeneza ndege ya kwanza iliofanikiwa iliokuwa inatumia injini na iliweza kuruka umabali wa mita 36 ndani ya sekunde 12.

 Orville Wright akiwa amefanikiwa kutua kwa mara ya kwanza ndege yao kaka yake Wilbur akimwangalia

Wilbur (kulia) na Orville (kushoto) Wright 
wakiwa wameketi katika ndege yao. 

Mwaka 1909 kwa mara ya kwanza Louis Bleriot alikuwa mtu maarufu duniani baada ya kufanikiwa kuruka na ndege alio itengeneza Km 40 ndani ya dakika 36 na pia aliafanikiwa kuanzisha kiwanda chake cha kutengeneza ndege.

Louis Charles Joseph Blériot

ndege ya kwanza ya Bleriot mwanzon mwa miaka ya 1909.

Mwaka 1919 ndipo biashara ya usafiri wa anga ilianza rasmi baada ya kuwepo na ndege zenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu . Baadhi ya  makampuni yalioanzishwa kwa ajili ya kusafirisha watu ni KLM kutoka Holland ambao mbaka sasa wanafanya vizuri sana katika usafirishaji wa anga, Avianca kutokea Spain walianzisha ruti ya kwenda Colombia, Farman Company ,Air France pamoja na Air transport.




 ndege ya kwanza kabisa kutumika kubeba abiria

 abiria wakiwa wanaingia ndani ya ndege tayari kwa safari

 Mwaka 1952 tekinolojia ya ndege iliongezeka zaidi baada ya kufanikiwa kugundua jet injini (injini za mitungi) ambazo ni bora na zenye nguvu zaidi na uwezo wa kufanya kazi kwa mda mrefu. Mbaka sasa usafiri wa anga umekuwa wa haraka na wakuaminika na makampuni mengi yamewekeza katika usafiri huo kutokana na kuwa na faida kubwa sana ,

Dubai international Airport ni moja ya Airport kubwa dunian na ubokea ndege nying kwa siku.

             Amstardam Airport Schiphol Baadhi ya ndege za shilika la KLM zikipakia na kushusha watu katika gates.

Bila shaka naamini umejinza kitu kupitia hii makala fupi ,pia usiache kuendelea kutembelea blog yetu ili upate kujifunza zaidi mambo ya anga Asante .




Comments

  1. jambo jema kuendeleza masomo juu yetu wafatiliaji wa mtadaoni

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WASANII AFRICA WANAO MILIKI PRIVATE JET.