USICHO KIJUA KUHUSU BOMBARDIER Q400 DASH 8 (AIR TANZANIA)
Ndege aina ya Bombardier Q400 dash 8 (turbo props engine) zinatengenezwa Canada na kwa mara ya kwanza ndege hii ililuka mwaka 1983 na mbaka sasa kampuni ya bombardier imefanikiwa kuuza ndege 1232 Tanzania ikiwa moja ya nchi inayo miliki ndege mbili aina ya Bombardier Q400. Ndege hii ilitengenezwa mahususi kwa ajili ya kupunguza gharama za uendeshaji na ina uwezo wa kuchukua abiria 78
na pia ina uwezo wa kutua kwenye uwanja mfupi na kuluka kwenye uwanja
mfupi kutokana na uwezo wake wa injini.
mpangilio wa siti ndani ya bombardier Q400 na ndege hii huwa na Cabin crew(Hosters) wawili kwa ajili ya kuhudumia abiria.
Turboprops (panga sita) aina ya injini ambayo hutumiwa na Bombardier.
Rwanda ni moja ya nchi ambayo utumia ndege hizi kwa muda mrefu sasa.
Naamini umejifunza kitu kupitia hi makala fupi ya ujue ndege aina ya Bombardier Q400 Dash 8. Usikose mfululizo wa vipindi ambao nitakuwa nautoa kupitia blog hii..



Comments
Post a Comment