TOFAUTI KATI YA BOEING NA AIRBUS
Je unaweza kuniambaia tofauti kati ya Airbus na Boeing?
Ma Pilot na watu wanao fatilia maswala ya anga ni rahisi sana kuzitofautisha ndege hizi zikiwepo zimepaki ata zikiwa angani, na Sio rahisi kwa watu wa kawaida..
Ndege aina ya Airbus ni ndege ambazo zime buniwa na zinatengenezwa na Muunganiko wa nchi za Ulaya (European multinational) na kuuzwa duniani kote.
Ndege aina ya Boeing ni ndege zime buniwa na zinazotengenezwa America na pia zinauzwa duniani kote. Boeing wamejikita katika kutengeneza ndege za abiria ,za kijeshi rocketi pamoja na satellites.
HIZI NDIO TOFAUTI KUBWA KATI YA BOEING NA AIRBUS
ukiangalia Pua ya Boeing imechongoka sana, pia ukiangalia madilisha ya Boeing ni pembe nne.
ukiangalia pua ya Airbus ina kuwa na umbo la yai pia ukiangalia madirisha utagundua kuna utofauti mkubwa sana.
ukiangalia mwisho wa bawa la Boeing utaona winglets kama hii.
ukiangalia kwenye bawa la Airbus utaona Sharklets kama hii.
bila shaka kupitia page hii utakuwa umepata mwanga na kuweza kutofautisha ndege hizi.

Comments
Post a Comment